Mh. Makalla afungua kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake Barani Afrika.


IMG_3481
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla akiingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake Barani Afrika lililofanyika katika Hoteli ya Peacok  Jijini Dar es Salaam.
IMG_3490
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,  Profesa Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla (Kulia) wakati wa Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake lililofanyika  Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mfuko wa Anita Foundation Dr. Anita White. 
IMG_3503
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla akifungua Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake lililofanyika  Jijini Dar es Salaam.
IMG_3510
Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa katika kongamano hilo  Jijini Dar es Salaam.
IMG_3556
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, anayefuata kushoto ni Mkuu wa Mfuko wa Anita Foundation Dr. Anita White, kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo, na anayefuata kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Shirika la Right to Play Afrika Bw.Denis Bright, waliosimama nyuma ni wachezaji wa Twiga Stars ambao pia wameshiriki katika Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake lililofanyika  Jijini Dar es Salaam.
Previous
Next Post »