Kushoto ni kijana aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka,kulawiti na kutoboa macho watoto
Kulia ni Jacob Mayani kinara wa ubakaji,ulawiti na kutoboa macho watoto Shinyanga
Mtuhumiwa aliyekuwa akikabiliwa na kesi za ubakaji na kulawiti watoto katika Manispaa ya Shinyanga amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kesi tatu tofauti.
Mtuhumiwa huyo Jacob Mayani au maarufu kwa jina la Boy mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa manspaa ya Shinyanga amehukumiwa vifungo vitatu vya maisha kwenye MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Mfawidhi Shinyanga.
Jacob Mayani ambaye alituhumiwa kuhusika na matukio tofauti ya ubakaji na kulawiti watoto chini ya miaka 10 sanjari na kuwatoboa macho amejikuta akiishia gerezani.
EmoticonEmoticon