AzamTV yaanza rasmi kuuza ving’amuzi vyenye chaneli 50 jijini Dar

 

MMG20240
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa makao makuu ya ofisi za Azamtv, yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam . Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington akishuhudia tukio hilo.
MMG20251
Sasa imezinduliwa rasmi.
DSC_0881
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Ofisi za  Azam TV na kusisitiza umuhimu wa kupanua wigo wa upatikanaji wa Chaneli zao 50 na kutoa huduma bora zenye ubora wa hali ya juu katika kuwafikia wateja wote wa ndani na nje ya nchi.
AzamTV  imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Huduma za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenye kisimbuzi kungalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa mwezi.
 Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo ni:
-Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
-Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia 
-SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Kwa pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya michezo, tamthilia, watoto na maisha.
Ofisi imefunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd.
“Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa
DSC_0897
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington,  akisisitiza upatikanaji wa vinga’muzi vya Azamtv kwamba vitapatikana maeneo karibu yote ya Tanzania Bara na Visiwani kwa manufaa ya watanzania wote.
Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV  ipo sokoni kwa ajili ya kila mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”
Azam Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa Tanzania.
DSC_0820
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akionyesha cake maalum iliyoandikwa “Azam Tv” ikiwa ni mbwembwe za kusherehesha uzinduzi  wa makao makuu ya ofisi za Azamtv, yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
DSC_0825
Wageni waalikwa wakijisevia cake mara baada ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Azam Tv ziliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam
DSC_0834
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akisalimiana na baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria uzinduzi huo 
DSC_0835
DSC_0839
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington, akisalimiana na wasanii wakongwe wa Bongo Movie kwenye sherehe za uzinduzi wa Ofisi za Azamtv 
DSC_0844
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau ambaye alimpongeza kwa hatua nzuri ya kuleta mapinduzi kwenye ulimwengu wa Digitali.
DSC_0846
Dr. Cheni akibadilishana mawazo na msanii mwenzake wa Bongo Movie Natasha, huku Msanii Batuli akishow love 
DSC_0851
Wasanii wa Bongo Movie katika picha ya pamoja huku nyuso zao zikiwa zimejaa furaha tele mara baada ya kuzinduliwa kwa Ofisi za Azamtv zilizopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
DSC_0890
Msanii Monalisa na Batuli 
DSC_0900
Wafanyakazi wa Azamtv kitengo cha Huduma kwa wateja wakiwa tayari kuwahudumia wateja wao walionaza kumiminika kwenye makao makuu ya Ofisi mpya za Azamtv zilizopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
DSC_0904
Baadhi ya wateja wakiwa wamejipumzisha kwenye Ofisi za Azamtv kusubiri kupewa huduma.
DSC_0909
Vijana watanashati na nadhifu wakiwa tayari kuwahudumia wateja wao.
DSC_0926
Mdau Othman Michuzi (kushoto) akipewa maelezo ya Chaneli mbalimbali zaidi ya 50 zinazopatikana kwenye King’amuzi cha Azamtv.
Previous
Next Post »