Maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika



jkuhuru



Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika uliopatikana Desemba 9, 1961.

Miaka 52 imetimia tangu Tanganyika (sasa Tanzania), kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza, Desemba 9, mwaka 1961.

Maadhimisho haya yamefanyika uwanja wa uhuru hapa Dar es salaam,Rais Jakaya Kikwete amekagua gwaride la vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama ambavyo pia vimetoa heshima kwa kiongozi huyo kwa mwendo wa pole na haraka.kikosi cha anga pia kimetoa heshima zake na burudani mbalimbali ikiwamo ngoma na michezo ya halaiki. 

Sherehe hizi zimehudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wa ndani na nje ya nchi, wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Katika maadhimisho haya kwa mwaka jana, yaliyohudhuriwa na viongozi 14 wa kutoka 

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Kikwete aliwataka Watanzania kujivunia na kuyaenzi mafanikio ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyopatika tangu nchi ilipopata uhuru. 


Previous
Next Post »