FAHAMU UMUHIMU WA KUNYWA MAJI KWA AFYA YAKO



 Kunywa maji ni muhimu sana kwa afya yako, ukiweza kunywa maji kwa siku katika kiwango kinachotakiwa kiafya utakuwa umejiepusha na matatizo mengi ambayo mengine ungelazimika kumeza vidonge kama vya kupunguza maumivu (pain killers) na matatizo mengine yanayohusiana na uchovu wa mwili.
Kabla ya kuoredhesha faida mbalimbali ni vizuri ujue, je kama ukipungukiwa na maji mwilini ni athari au mataizo gani unayopata? Ukipungukiwa na maji mwilini unaweza kujisikia uchovu, kichwa kuuma, ngozi kukakamaa kutokana na kukauka, chakula kutosagwa vizuri ambapo unaweza pata shida kujisaidia haja kubwa na kadhalika.
Vilevile kama ukipungukiwa na maji mwilini utaweza kuwa na hizi dalili,

  •  Kuhisi kiu au wakati mwingine hata kwikwi.

  • Kuhisi njaa. (Watu wengi hudhani kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kula chakula, lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine kuhisi ni dalili ya kutakiwa kunywa maji.)

Swali la kujiuliza ni, je unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa siku? Wataalamu wa afya wanashauri unywe maji angalau glasi 8 (250ml) sawa na lita 2 kwa siku.
Baada ya kujua dalili za ukosefu wa maji mwilini pamoja na matatizo utakayopata kama hutokunywa maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili wako. Napenda ujijengee hizi tabia nzuri za kiafya wakati unapohitaji kunywa maji…

  • Kila uamkapo asubuhi kunywa angalau glasi moja (1) ya maji.

  • Kila unapotaka kula, kunywa maji kabla ya kuanza kula chakula chako. Vilevile kunywa maji wakati ukiendelea kula na mwisho wa kula chakula kunywa maji tena.

  • Kabla ya kuanza kufanya mazoezi pendelea kunywa maji kwanza. Kunywa maji glasi 1 au 2 dakika 30 kabla ya kuanza kufanya mazoezi.
Hakikisha unajijengea tabia nilizozitaja hapo juu, ni rahisi ukishapata mazoea ya kufanya hivyo kila unapotaka kunywa maji. Kwa kuwa maji ni muhimu na yanakazi nyingi sana mwilini, zifuatazo ni faida za maji mwilini kiafya.

1. Maji husaidia kuboresha ngozi.
-Seli za ngozi zinahitaji maji kwaajili ya kazi zake zikiwemo kulinda ngozi kwa kupambana na magonwa mbalimbali yakiwemo eczema, psoriasis na hata makunyanzi na kukauka kwa ngozi. Hivyo ukitaka kuoenekana mwenye ngozi nzuri kama ya mtoto penda kunywa maji kwa kiwango kinachotosha.

2. Maji husaidia katika utendaji kazi wa ubongo.
-Ukitaka kuwa mwenye akili safi na mwepesi wa kufikiri na kutatua mambo mbalimbali yanayohitaji kutumia akili, basi penda kunywa maji pamoja na vyakula vyenye kusaidia seli za ubongo kufanya kazi zake vizuri. Ubongo unahitaji maji, hewa safi ya oxygen na vyakula vyenye virutubisho kama njugu mawe, mafuta ya samaki (fish oil), nyanya na mbegu za maboga.

3. Maji husaidia usagaji wa chakula.
-Mfumo wa umeng'enyaji wa chakula (digestive system) hutegemea sana maji katika ulainishaji wa chakula na hivyo kuwezesha virutubisho vya chakula kutumika vizuri na mwili, kwakuwa maji hulainisha chakula, pia huepusha kupata choo kigumu (constipation).

4. Maji husaidia kuondosha sumu na taka mwilini.
-Licha ya maji kuwa ni sehemu kubwa ya miili yetu pia ni kitu ambacho kinawezesha viungo vingine muhimu sana kama moyo katika usukumaji damu yenye kiwango kikubwa cha oxygen ambayo inabeba maligafi nyingi sehemu mbalimbali za mwili na figo katika uchujaji wa taka za mwili.

5. Maji husaidia kupunguza maumivu mbalimbali kama ya kichwa pamoja na mgongo.
-Licha ya kuwa na sababu nyingi za mtu kupata maumivu ya kichwa lakini pia ukosefu wa maji mwilini ni sababu moja wapo.

6. Maji huusaidia mwili kupigana na magonjwa mengi kama ya mafua, tumbo, saratani za aina mbalimbali na matatizo mengine ya figo.
-Maji pamoja na juisi ya malimao husaidia sana kupooza magonjwa kama ya kikohozi, mafua, kuchafuka kwa tumbo, satani ya tumbo na kibofu cha mkojo nakadhalika. Maji yanaweza kukuepusha au kupunguza makali ya magonjwa hayo kwa kusaidia mwili wako kuongeza kinga ya mwili.

7. Maji husaidia kupunguza uzito.
 -Kama nilivyosema hapo awali wakati mwingine unaweza hisi kuwa unahitaji kula kumbe unahitaji kunywa maji kwakuwa umepungukiwa na maji mwilini. Ni mara ngapi umekuwa ukitamani kula chakula kwa pupa lakini baada ya kunywa maji ukajikuta unakula kidogo kuliko ulivyotegemea hapo awali. Uzito wa mwili hutegemea sana ulaji wa chakula pasipo kufanya mazoezi, maji pia husaidia kuondoa taka za vyakula vya mafuta (fats by-products) na kukuwezesha uwe mwenye afya bora.

8. Maji husaidia kuboresha misuli na kulainisha jointi za mwili.
-Maji pia ni chanzo cha nguvu mwilini, misuli huifadhi nguvu za ziada zitakazo tumika iwapo nguvu ya mwili itapungua. Kunywa maji kulingana na mwili wako unavyohitaji ili kuwezesha utumikaji mzuri wa chakula na uhifadhi wa uhakika wa nguvu ya mwilini. Maji pia yatakusaidia kulainisha viungo vyako vya mwili kama jointi za kwenye magoti, vidole vya mikono na miguu nakadhalika.

Previous
Next Post »