Fat Joe Atoka Jela Mapema Na Kumshangaza Mtoto Wake



Fat Joe ametoka jela mapema kuliko ilivyotegemewa na kumshangaza mtoto wake kwenye Thanks Giving. 

Rapper Fat Joe ametoka jela na kushangaza familia yake akiwemo mtoto wake wa kike baada ya kutokea nyumbani siku ya Thanks Giving. Joseph Cartagena alikuwa anatumikia kifungo cha miezi minne kwenye jela iliyopo Miami kwa kosa la kukwepa koda.

 Mnamo tarehe 26 August 2013 Joe alijisalimisha Miami Federal Detention Center kutumikia kifungo chake na jumatano hii alitoka na kwenda moja kwa moja nyumbani kwake. Taarifa za kutoka mapema kwa Joe zilisikika kutoka kwa producer wa All I Do Is Win, Producer DJ Nasty.
Previous
Next Post »