Chatu mmoja mkuwa amewaua watoto wawili mashariki mwa Canada waliokuwa wamelala.
Watoto
hao wa kiume Noah Barthe aliyekuwa na umri wa miaka mitano na kaka yake
Connor wa miaka saba, walikuwa wajipumzisha katika nyumba ya rafiki yao
mpendwa katika mji wa Campbellton wakati walipovamiwa na chatu huyo
aliyetoroka katika duka la wanyama lililoko gorofa ya kwanza ya nyumba
hiyo.
Polisi wamesema chatu huyo aliingia katika nyumba hiyo kupitia katika mabomba ya mfumo wa kuingiza hewa ndani.
Watoto hao walikuwa wamelala katika sebule ya nyumba hiyo.
EmoticonEmoticon