“PRESS
RELEASE” TAREHE 06. 08. 2013.
WILAYA
YA ILEJE - MAUAJI
MNAMO TAREHE 05/08/2013 MAJIRA YA SAA 17:00
HUKO KIJIJI CHA IBABA WILAYA YA ILEJE NA MKOA WA MBEYA. MTOTO JOSHUA S/O
MWAMPAMBA ,4YRS , MNDALI NA MKAZI WA KIJIJI CHA IBABA ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI
NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI
WAKE NA MIKA S/O KISUNGA ,20YRS, MNDALI NA MKAZI WA KIJIJI CHA IBABA. MTUHUMIWA
AMEKAMATWA PAMOJA NA KUWA NA MATATIZO YA AKILI, MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA
UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA
KUKABIDHIWA KWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA NA UANGALIZI
MAALUMU KWA WATU WENYE MATATIZO YA AKILI ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA
KUJITOKEZA .
WILAYA
YA CHUNYA – KUJERUHI
MNAMO TAREHE 05/08/2013 MAJIRA YA SAA 24:30
HRS HUKO KIJIJI CHA MWAMBANI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. DAFROSA D/O
SAIDIA, 30YRS MNYAMWANGA, MKULIMA ALICHOMWA KISU UPANDE WA KULIA WA TUMBO NA
UTUMBO KUTOKA NJE NA MTUHUMIWA AMBAYE NI MPENZI WAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA NJELE S/O LUHENDE ,MKAZI WA MWAMBANI.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MHANGA
AKIWA AMEKAA BAA NA MWANAUME MWINGINE. MTUHUMIWA ALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO
HILO NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI TEULE YA MWAMBANI CHUNYA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUTATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO YA KIJAMII KWA NJIA YA MAZUNGUMZO ILI KUJIEPUSHA
NA MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
WILAYA
YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 05.08.2013 MAJIRA YA SAA
14:00HRS HUKO ENEO LA KALUNGU KIJIJI CHA MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA NA MKOA
WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA ANNA D/O MWAKALINGA ,30 YRS,KYUSA,MKULIMA NA MKAZI WA KALUNGU AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 15. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO TARATIBU
ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA SAMBAMBA NA KUWA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA
MNAMO TAREHE 05.08.2013 MAJIRA YA SAA 12:30
HRS HUKO KIJIJI CHA ISANZU WILAYA YA CHUNYA NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JACKSON S/O LAIN, 61YRS, MNYIHA, MKULIMA NA MKAZI WA
ISANZU AKIWA NA BUNDUKI AINA YA GOBOLE .MBINU NI KUFICHA SILAHA HIYO JUU YA
DARI NDANI YA NYUMBA YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUMILIKI SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI KOSA LA JINAI.
WILAYA
YA RUNGWE - KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 05.08.2013 MAJIRA YA SAA
14:00HRS HUKO ENEO LA KK WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA
WATUHUMIWA WATANO [5] AMBAO NI [1]
MAJALIWA S/O HERIOT, 21 YRS,KYUSA,
MKULIMA NA MKAZI WA KK, [2]
RAMADHANI S/O MAJID ,25 YRS , MPERE,MWANAFUNZI WA SEKONDARI NA MKAZI WA KK,[3] IMANI S/O ALLY ,22YRS,KYUSA,MKULIMA
WA KK TUKUYU [4] IPYANA S/O
GIDION,23 YRS KYUSA MKULIMA WA KK NA [5] ISAYA S/O GIDION,21 YRS,
KYUSA,MKULIMA WA KK WAKIWA NA MISOKOTO 32,
KETE 34, NA GRAMU 7 ZA BHANGI AMBAZO NI SAWA NA UZITO WA GRAMU 337. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI
WA BHANGI HIYO TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA [BHANGI] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA SAMBAMBA NA KUWA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
Signed
By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon