Msanii Tundaman baada ya mwezi
wa Ramadhani na sherehe za Eid kukamilika, amejipanga kufanya
mashambulizi ya nguvu kwa kuachia kazi kubwa tatu ambazo zitawapatia
mashabiki kile walichokimiss kwa muda mrefu kutoka kwake.
Tundaman amewataka mashabiki wa kazi zake kujiandaa na video mpya
ya Kaswida kutoka kwake, Video ya ngoma yake ya Wanaona Haya, na
vilevile mkono mpya kabisa ambao ndio unamalizika studio, mkono ambao
ndani yake anatarajia kusikika Bidada Recho.
EmoticonEmoticon