Prezzo kukutana na Jay Z


Rapa Prezzo ambaye hivi sasa yupo katika ziara nchini Marekani ambapo anatarajia kwa mara yake ya pili kukutana na gwiji wa rapa nchini humo rapa Jay Z katika mwaliko maalum wa kampeni za kutokomeza njaa barani Afrika ameelezewa kuwa hakufanikiwa kupata idadi kubwa ya mashabiki katika shoo zake nchini humo.
Imeelezwa kuwa Prezzo alikuwa na maonyesho ya muziki katika miji ya Dallas, Texas nchini Marekani ambapo pamoja na umaarufu wake mkubwa aliokuwa nao lakini hakuweza kupata mashabiki wengi ambapo idadi ya  waliotinga ukumbini walifikia watu 30 tu.

Aidha, pamoja na hayo yote Prezzo anajivunia kuwa ameweza kukubalika na baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa pamoja na mkali huyo tangu alipopata umaarufu wa ushiriki wake katika shindano maarufu la kipindi cha televisheni cha maisha uhalisia nchini Afrika Kusini.
Previous
Next Post »