“PRESS
RELEASE” TAREHE 05. 08. 2013.
WILAYA YA MBARALI – AJALI
YA MAGARI MAWILI KUGONGANA
NA KUSABABISHA KIFO.
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 04.08.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO MSWISWI WILAYA YA MBARALI
BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI
YA HOOD LIKIENDESHWA NA DEREVA OMARY
S/O SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014
TOYOTA COROLLA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS S/O ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA
MKAZI WA MUNZE LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO PAPO HAPO. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI NA DEREVA WA HOOD BUS AMEKAMATWA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI
– MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 04.08.2013 MAJIRA YA SAA 18:40HRS HUKO IKUMBI-SONGWE WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI MKOA WA MBEYA. NASIBU S/O MATINYA, MIAKA 25, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA SONGWE
ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWA KUTUMIA MAPANGA, MAWE NA FIMBO KISHA KUMCHOMA MOTO. CHANZO NI TUHUMA ZA
WIZI BAADA YA MAREHEMU KUIBA MAHINDI DEBE 3 MAHARAGE BAKURI 10, DOTI 3 ZA
VITENGE NA PAMPU YA BAISKELI 1 NYUMBANI KWA HEBRON S/O MWAKIMONYA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE
KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE.
Imesainiwa
na,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon