“PRESS RELEASE” TAREHE 04. 08. 2013.
WILAYA YA MOMBA - MAUAJI
MNAMO TAREHE
02/08/2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI MKOA
WA MBEYA, MSAWILE S/O HALINGA, MIAKA 70, MKULIMA MNYIHA, NA MKAZI WA KIJIJI CHA
LUMBELA ALIUWA KWA KUKATWA NA SHOKA SEHEMU ZA MGONGONI, SHINGONI NA KICHWANI
AKIWA NYUMBANI KWAKE NA MKE WAKE AITWAYE ESTER D/O MGALA, MIAKA 60, MKULIMA,
MNYIHA NA MKAZI WA KIJIJI HAPO KUJERUHIWA SEHEMU ZA MKONO WA KULIA NA KICHWANI
WAKATI AKIJARIBU KUMSAIDIA MUMEWE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI
HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA, MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMWITA MAREHEMU SEHEMU ZA
KIZANI NA KISHA KUMSAMBULIA. JUHUDI ZA KWASAKA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO
HILO ZIENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA KUWAUWA
WAZEE/VIKONGWE KWA DHANA ZA KISHIRINA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA PIA ANATOA
RAI WA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO AZITOE KATIKA
MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA
DHIDI YAO.
WILAYA YA RUNGWE –
MAUAJI
MNAMO TAREHE
30-31/07/2013 MAJIRA YASIYOFAHAMIKA HUKO KIJIJI CHA MPUMBULI KATA YA MPUGUSO
WILAYA YA RUNGWE, LUKAS S/O MWAKYOMA, MIAKA 50, MNYAKYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA
KIJIJI CHA MPUMBULI ALIUAWA NA RAMADHANI S/O MWAKYOMA, MIAKA 45, MNYAKYUSA, MKULIMA
WA MPUMBULI NA GODWIN S/O MWAKYOMA, MIAKA16, MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI SHULE YA SEKONDARI MPUMBULI KWA
KUPIGWA NA FIMBO SEHEMU ZA KICHWANI NA KUVUNJWA SHINGO KISHA KUFUKIWA KWENYE
SHIMO LA UREFU WA FUTI MBILI {2}. MNAMO TAREHE 03/08/2013 MAJIRA YA SAA
16:00HRS MWILI WA MAREHEMU ULIGUNDULIWA NA KUFUKULIWA KISHA KUZIKWA UPYA BAADA
YA UCHUNGUZI WA DAKTARI. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA MASHAMBA NA
WATUHUMIWA WOTE WAMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHHUKULIA
SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE KUYATATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMMZO
ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA GARI
KUACHA NJIA/KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE
03/08/2013 MAJIRA YA SAA 17:35HRS HUKO MAENEO YA MLIMA NYOKA WILAYA YA MBEYA VJIJINI BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI
NO T.564 BPQ/T.941 BME AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA MOHAMED S/O ABUBAKAR, MIAKA 46, MPOGORO,
MKAZI WA DSM LILIACHA NJIA KISHA KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA
ASIFAHAMIKA NA MAJERAHA KWA WATU WATATU AMBAO NI :-{1} ATHUMANI S/O MWANKENJA,
MIAKA 39 MNYAKYUSA{2} ISAYA S/O SANGA, MIAKA 41, MKINGA, MKAZI WA UYOLE NA {3}
ANDREW S/O VUNGWA, MIAKA 34, MNYIHA NA MKAZI WA SOKOMATOLA, MAJERUHI WAMELAZWA
KATIKA HOSPIPTALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO
CHA AJALI KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA
Signed
by
[DIWANI
ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon