Papa Francis akijibu maswali ya wanahabari wakati akirejea kutoka Brazil. ©AP
|
Ni siku moja mara baada ya kurejea kutoka kwenye siku ya vijana duniani,
tamasha la asili ya kanisa katoliki ambalo limefanyika mwaka huu nchini
Brazil. mara baada ya kurudi Ulaya, Papa Francis amezungumza na
waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika mkutano, na kunukuliwa
akizungumzia kuhusu watumishi mashoga.
Katika mkutano na waandihsi wa habari ambao umechukua takriban dakika 82
wakiwa angani, Papa Francis amesema kuwa hana shida na mtu ambaye ni
shoga na anamtumikia Mungu kikamilifu.
Nitanukuu kwa Kiingereza na kisha kutafsiri kwa kiswahili rahisi.
"If someone is gay and he searches for the Lord and has good will, who
am I to judge?" Francis asked. "We shouldn't marginalize people for
this. They must be integrated into society."
Yaani anasema, "Kama mtu ni shoga na anamtafuta Bwana na ana nia njema, mimi ni nani hata nihukumu?" Papa Francis anasema na kuongeza, "Hatupaswi kutanga watu kutokana na hili suala. Inabidi wakubalike na kuchukuliwa ndani ya jamii."
kauli ya Papa Francis inaonekana kukinzana na ile ya mtangulizi wake, Papa Benedick XVI, ambaye mnamo mwaka 2005
, alisaini waraka wa kueleza kuwa wanaume
wanaojihusisha na masuala ya ushoga, hawatakiwi kuwa makuhani. Kwa
mujibu wa Papa Francis, mtazamo wake ni kwamba watumishi mashoga
wasamehewe na dhambi zao zisahauliwe.
Hata hivyo licha ya mtazamo huo wa Papa. Bado sera ya kanisa katoliki
hairuhusu masuala kama hayo, ila kutokana na kauli ya kiongozi huyo mkuu
wa kanisa katoliki, huenda kukawa na mabadhiliko kwenye mtazamo wa
kanisa kuhusu jambo hilo.
Chama kikubwa cha kupigania haki za mashoga nchini Marekani, Human
Rights Campaign - wameonekana kufurahishwa na kauli ya Papa, na kusema
kuwa, "kwa miaka kadhaa sasa tumeona mashoga na wasagaji wanaotokea
Vatican wakikandamizwa, kauli ya Papa inaleta matumaini angalau."
Anaeleza Rais wa chama hicho, Chad Griffin.
Katika hatua nyingine Papa Francis alizungumzia kuhusu wanawake kuwa na
jukumu zaidi katika kanisa, lakini kusema kuwa bado hawawezi kuwa
wachungaji/makuhani.
Papa Francis
akishuka kutoka kwenye ndege mara baada ya ndege kutua kwenye uwanja wa
ndege wa kivita wa Ciampinos, pembezoni mwa Rome wakati akirejea kutoka
Brazil tarehe 29 Julai 2013. ©AP
|
EmoticonEmoticon