Ndizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana
karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa
tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako
kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku
moja .
Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari
hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose ,
Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu
ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu
inayohitajika mwilini mwako .
Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati
ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa
moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu
kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya
mashindano katika mchezo husika .
Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili
lina faida nyingine ambayo ni kuusaidia mwili wako kupambana na
kujikinga na maradhi kadhaa. Msongo wa Mawazo/Mfadhaiko wa akili(stress & Depression)
Kwa mujibu wa tafiti kadhaa , watu wengi wanaopata mafadhaiko au
msongo wa mawazo hujisikia nafuu pale wanapokula ndizi mbivu . Hii ni
kwa sababu ndizi mbivu zina virutubisho aina ya TRYPTOPHAN ambayo ni
aina ya protini ambayo mwili huigeuza na kuwa SEROTONIN ambayo kazi yake
ni kukufanya upate utulivu na kukurejesha katika hali ya kawaida mpaka
utakapota furaha na kuondokana na msongo wa mawazo . Zaidi ya hapo ndizi
huongeza Vitamini B6 mwilini ambayo inasimamia usambazaji wa glucose
au sukari mwilini na hivyo kusaidia kutuliza msongo wa mawazo .
Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
Ndizi zina madini ya chuma na zinasaidia uzalishaji wa haemoglobin
ambayo ni mzalishaji mkuu wa damu mwilini hivyo inawasaidia wale wenye
matatizo ya upungufu wa damu mwilini.
Presha ya Damu.
Ndizi mbivu zina madini ya Potasium na ina madini ya chumvi kwa
kiwango cha chini jambo ambalo linafanya tunda hili kuwa dawa ya
kupambana na matatizo ya presha . Mamlaka ya chakula na dawa nchini
marekani imetambua uwezo wa ndizi katika hili kiasi cha kuagiza
wazalishaji na viwanda vya ndizi kufanya tunda hili kuwa rasmi katika
mapambano ya kupunguza vifo vitokanavyo na presha na kiharusi(stroke)
Nguvu ya Ubongo/Akili(Brain Power)
Katika utafiti uliofanywa huko Twickenham (Middlesex) nchini
Uingereza wanafunzi 200 walifaidika kwa kufaulu mitihani yao mwaka huu
kwa kula ndizi mbivu katika milo ya asubuhi na mchana . Ndizi
imebainika kuwa na uwezo wa kuusaidia ubongo kuongeza nguvu yake .
Utafiti umeonyesha kuwa madini ya Potassium yanaweza kusaidia ubongo
kuwa na kasi na uwezo zaidi ya hali ya kawaida . Kufunga Choo(Constipation)
Fiber inayopatikana kwenye ndizi mbivu inaweza kuurejesha utumbo ambao umesababisha kufunga choo kufanya kazi kama kawaida .
Madhara ya matumizi ya kilevi(Hangover)
Moja ya njia za haraka za kurudi kwenye hali ya kawaida baada ya
kupata madhara ya matumizi ya kilevi hasa asubuhi unapoamka ni kutumia
ndizi au bidhaa zitokanazo na ndizi kama vile Banana Milkshake . Ndizi
hutuliza tumbo na inajenga au kurejesha kiwango cha kawaida cha sukari
mwilini huku ikirutubisha mfumo wa maji mwilini .
Kiungulia (Heartburn)
Ndizi zina uwezo wa kupambano na kemikali au acid zinazosababisha kiungulia , jaribu kula ndizi na utakuwa shahidi katika hili.
Kuumwa asubuhi kwa kina mama wajawazito(Morning Sickness)
Matumizi ya ndizi yamegundulika kusaidia kuepusha kuugua asubuhi
ambako kunawapata kinamama wajawazito , hii ni kutokana na uwezo wa
tunda hili wa kucontrol kiwango cha sukari mwilini.
Alama za Kung’atwa na Mbu.
Kwa wale wanaotokwa na vile vipele vidogo vyekundu baada ya kung’twa
na mbu , jaribu kufuta eneo lenye kipele kama hicho kwa upande wa ndani
ya ganda la ndizi , ni ajabu lakini hufanya kazi kwa kuwa hii hupunguza
uvimbe na muwasho.
Neva (Verves)
Ndizi zinasaidia sana kutibu mfumo wa neva (nervous system).
Hata kwa wale watu wenye matatizo ya uzito ambao unatokana na tabia
zisizo za salama za ulaji hasa kutokana na kukosa muda wa kula na
kulazimika kula vyakula vyenye mafuta mengi vinavyopikwa haraka ndizi
inaweza kuwa msaada mkubwa . Utafiti uliofanywa kwa watu 5000 ambao
walikuwa wagonjwa wa hospitalini walipata nafuu ya matatizo yao kwa
kutumia ndizi kila baada ya saa mbili .
Vidonda vya tumbo .(Ulcers)
Ndizi zinatumika kama chakula ambacho kinaweza kuwa na msaada kwa
watu wenye matatizo kwenye utumbo, hii ni kutokana na ulaini wake na
hupunguza acid ambayo inasababisha vidonda tumboni na pia hupunguza
maumivu kutokana na kuziba baadhi ya vidonda hivyo .
Kupunguza hali ya joto mwilini.
Ndizi ni tunda ambalo huweza kusaidia kupunguza joto . Nchini
Thailand kina mama waja wazito hula ndizi ili kuhakikisha wanawazaa
watoto wao katika hali ya joto pungufu .
Hivyo basi ndizi ni tunda ambalo lina uwezo wa kusaidia matatizo
mengi ya afya ya mwanadamu . Unapolifananisha na Apple ndizi inazidi
tunda hili kwa protini kwa angalau mara nne , madini ya wanga au
carbohydrates mara mbili , madini ya fosforasi mara tatu ,Vitamini A na
madini ya chuma mara tano , na mara mbili kwenye vitamin nyingine na
madini . Ni muda wa kubadili ule msemo usemao Apple moja kwa siku
hukuweka mbali na daktari na kuufanya kuwa Ndizi moja kwa siku hukuweka
mbali na daktari au hospitali.
EmoticonEmoticon