
Rais wa Zanzibar Dkt Shein, akwaapisha Mawaziri na Manaibu Katibu Wakuu na Manaibu wake, Ikulu.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya
Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya
baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Kufuatia
marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na
kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika Wizara
nyengine. Marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo
zinaendelea kubaki Wizara 16.Shughuli
za Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ zimeondolewa katika Ofisi ya
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kuundiwa Wizara mpya.
Shughuli za Utawala Bora zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Shughuli za kazi zimeunganishwa na shughuli za utumishi na kuundiwa Wizara mpya.
Shughuli za uwezeshaji
wananchi kiuchumi na ushirika zimeondolewa kutoka Wizara ya Kazi,
Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi na Ushirika na kuunganishwa na shughuli
za ustawi wa jamii, vijana, wanawake na watoto.
Shughuli za Tume ya Mipango
zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi.
Aidha, kufuatia kuundwa kwa
Wizara hizo mpya Rais Dk. Shein amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la
Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Wizara kwa kuwabadilisha Wizara baadhi
ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Ikulu na Utawala Bora anakuwa Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame na katibu
Mkuu wake anakuwa ndugu Salum Maulid Salum ambapo Naibu Katibu Mkuu
ofisi hiyo anakuwa Said Abdulla Natepe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, anakuwa Mhe. Haji Omar
Kheir na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anakuwa ndugu Joseph Meza ambapo
Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa ni ndugu Mwinyiussi A. Hassan na Naibu
Katibu Idara Maalum za SMZ anakuwa CDR Julius Nalimy Maziku.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Kazi na Utumishi wa Umma anakuwa Mhe. Haroun Asli Suleiman na
Katibu Mkuu wake anakuwa ndugu Fatma Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma anakuwa ndugu Yakout Hasan Yakout.
Wizara ya Fedha itakuwa
chini ya Waziri Mhe. Omar Yussuf Mzee na Katibu Mkuu wake
ni ndugu Mussa Omar na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo atakuwa ndugu
Juma Ameir Hafidh.
Waziri wa Uwezeshaji,
Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto anakuwa Mhe. Zainab Omar
Mohamed ambapo Katibu Mkuu wake atakuwa ndugu Asha Ali Abdalla na Naibu
Katibu Mkuu Uwezeshaji na Ushirika atakuwa ndugu Ali Khamis Juma na
Naibu Katibu Mkuu Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto atakuwa
ndugu Msham Abdalla Khamis.
Wakati huo huo, Dk. Shein amewaapisha viongozi hao jana jioni.
EmoticonEmoticon