Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee
Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Spika wa Bunge
Mhe. Anne Makinda, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na
viongozi wengine wakiwa katika msiba wa binti wa Makamu Mwenyekiti wa
CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam
jana Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi iliyopita kwa
ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kwenda Njombe
kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa heshima
zao za mwisho kwa marehemu Nemela Phillip Mangula, binti wa Makamu
Mwenyekiti wa CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini
Dar es salaam jana Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi
iliyopita kwa ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013.
EmoticonEmoticon