Polisi
nchini Zanzibar wameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 10 za
Tanzania kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa
watu waliowashambulia wasichana wawili waingereza kwa Tindikali.
Wasichana hao kutoka London, Kirstie
Trup na Katie Gee, walirushiwa Tindikali kwenye nyuso zao walipokuwa
wanatembea mjini Jumatano Jioni.
Serikali ya Zianzibar ndio itakayotoa zawadi hiyo. (HM)
Polisi wanasema kuwa hizo ni pesa nyingi sana kisiwani Zanzibar.
Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye
umri wa miaka 18 kutoka London, walipelekwa hospitalini nchini Tanzania
baada ya kushambuliwa Mashariki mwa kisiwa hicho.
Inaaminika kuwa walitoka Tanzania kuelekea Uingereza Alhamisi usiku.
Mama za wasichana hao, Rochelle Trup
na Nicky Gee, walielezea kughadhabishwa mno na shambulizi hilo ambalo
sababu yake haiwezi kujulikana na ambalo halikuchochewa kivyovyote.
Walishambuliwa na wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
Polisi walisema kuwa walirushiwa Acid kwenye nyuso zao, kifuani na kwenye mikono yao walipokuwa wanatembea mjini .
Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliowashambulia walitoroka na polisi hawajui kwa nini wanawake hao walilengwa.
Mama za wasichana hao walisema kwenye
taarifa yao kuwa walighadhabishwa mno na shambulizi hilo na hawaelewi
kwa nini wasichana hao walishambuliwa ili hali walikwenda Zanzibar kwa
nia njema.
''Tunashukuru kwa wale wanaotaka kujua
kinachoendelea lakini tungeomba vyombo vya habari vituwache kwa sasa
hadi tutakapokutana na watoto wetu,'' alisema msemaji wa familia za
wasichana hao.
Wasichana hao walikuwa wamekaa
Zanzibar kwa muda wa wiki mbili ingawa walitarajiwa kuwa huko kwa wiki
tatu, kupitia kwa kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel, ambayo ilisema
inafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani Uingereza.
Kari Korhonen, mkurugenzi mwenza wa
kampuni ambayo wasichana hao walikuwa wanafanyia kazi, alisema kuwa hali
yao si mbaya ikizingatiwa athari za Acid kwa mwili na visa ambavyo
vimewahi kushuhudiwa vya kuchomwa kwa Tindikali
Msemaji mwingine aliongeza kuwa
wasichana hao walikuwa njiani kuelekea kwa maankuli ya jioni wakati wa
shambulizi hilo.
Chanzo: bbcswahili
EmoticonEmoticon