Mtoto Aanza Kuongea Dakika Chache Baada ya Kuzaliwa



 

Mtoto mmoja nchini Urusi amewashangaza wazazi na madaktari baada ya kuanza kuzungumza dakika chache baada ya kuzaliwa. Kwa mujibu wa tovuti za nchini Urusi, mtoto huyo alianza kusema neno lake la kwanza punde baada ya kuzaliwa kwa kutamka kifasaha kwa kumuita baba yake "Baba!".

Na katika dakika chache baadae mtoto huyo aliyepewa jina la Stephan alitamka "Mama!".

Miujiza ya mtoto huyo haikuishia hapo kwani siku iliyofuatia wakati mama wa mtoto huyo alipomwambia mtoto huyo "Baba yako anakuja hospitali" kwa mshangao mtoto huyo alijibu "Nani?, Baba?".

Mama wa mtoto huyo Lisa Bazheyeva, mwenye umri wa miaka 17 na baba wa mtoto wake Rodion Bejeev wanaishi katika jiji la Norilsk nchini humo.

Madaktari waliomsaidia mama huyo wakati wa kujifungua wamethibitisha taarifa za kuongea kwa mtoto huyo.

"Nilisikia kwa masikio yangu mtoto huyo akiongea punde tu baada ya kuzaliwa" alisema Dokta Marina Panova, na kuongeza "Sijawahi kuona kitu kama hiki katika miaka yangu 23 ya kufanya katika kliniki ya uzazi". 

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng