Mwanamke
maarufu zaidi duniani Oprah Winfrey amekumbana ana kwa ana na kile
anachokiita kitendo cha Ubaguzi wa rangi nchini Switzerland baada ya
muuza duka mmoja kukataa kumuuzia mkoba wa kike wa mkononi na kumwambia
kuwa hangeweza gharama yake.
Oprah ambaye ametajwa katika vitabu
vya Forbes kama mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa
duniani na
mmoja wa watu tajiri zaidi amedai kuwa msichana aliyekuwa akiuza hapo
dukani alimdharau kutokana na rangi yake. (HM)
Uswis imejikuta katika kizungumkuti na wanaharakati wa haki za binadamu.
Wiki iliyopita nchi hiyo ilitangaza
sheria katika baadhi ya mabaraza yake ya miji kuwa wahamiaji wa nje
hawataruhusiwa kutangamana na raia wenyeji hasa katika maeneo ya umma
kama vile mabwawa ya kuogelea, uwanja wa michezo na hata kanisani.
Sasa madai haya ya Oprah yanatoa taswira mbaya zaidi ya jinsi hali ilivyo nchini humo kuhusu ubaguzi wa rangi.
Wanaharakati wa haki za binadamu
wamesema kuwa hii ni ishara ya kuwa na ubaguzi ule uliowahi kutokea kwa
muda mrefu huko Afrika Kusini.
Oprah amesema kuwa aliondoka dukani
hapo taratibu bila kufanya vurugu lakini amesikitika kuona kuwa bado
ubaguzi wa rangi unaendelea na kuenea.
Mwaka jana pekee Oprah alikuwa na
fedha jumla ya dola za Kimarekani milioni sabini na saba na amesifiwa
kuwa mfanyibiashara tajiri, ambaye pia anamiliki shirika lake binafsi la
utangazaji na anafadhili miradi mingi ya misaada katika pembe mbali
mbali za dunia.
Alipata umaarufu wake kutokana na kipindi chake cha Oprah Winfrey Show kilichooneshwa nchi nyingi.
Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini
Zurich anasema kuwa kipindi hicho hakijawahi kupeperushwa katika runinga
za Switzerland na huenda sio wengi wanaofahamu Oprah ni nani huko.
Oprah alikwenda Uswis kuhudhuria harusi ya mwanamuziki Tina Turner.
Chanzo: bbcswahili
EmoticonEmoticon