WILAYA YA MBARALI –
MAUAJI.
MNAMO TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA
08:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MUHELA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. OSWARD
S/O YOHANA, MIAKA 17, MKINGA, DEREVA WA PIKIPIKI @ BODABODA MKAZI WA KIJIJI CHA
IGALAKO, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE
KISHA KUTELEKEZWA KWENYE MASHAMBA YA
MPUNGA. MAREHEMU ALIONDOKA
NYUMBANI KWAKE TAREHE 07.08.2013 JIONI AKIWA NA PIKIPIKI YAKE T.770 BYH
AINA YA SHINLEY AMBAYO IMEKUTWA ENEO LA
TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA YA KUKATWA MAPANGA AMBAPO VIDOLE VIWILI VYA
MKONO WA KUSHOTO VIMETOLEWA KWA KUKATWA, JICHO LA UPANDE WA KUSHOTO
LIMETOBOLEWA NA KUTOLEWA PIA MAJERAHA
MAKUBWA MANNE KICHWANI. CHANZO CHA TUKIO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU
KUTUHUMIWA KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MKE WA NIKOLAUS S/O DAMSON AMBAYE
NDIYE MTILIWA SHAKA NA AMETOROKA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU
UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI .KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO
WATUNWALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE
NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
|
WILAYA YA
MBARALI - AJALI YA TREKTA NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA
17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWAKAGANGA
WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. TREKTA
T.885 BPY LIKIWA NA TELA AMBALO HALINA NAMBA ZA USAJILI LIKIENDESHWA NA
ALEX S/O KALONGA, MIAKA 25, MKINGA, DEREVA MKAZI WA UBARUKU LILIMKANYAGA TEGEMEO S/O WILANGALI,MIAKA 29,
MBENA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
MWAKAGANGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO. CHANZO NI BAADA YA MAREHEMU KUJARIBU KUDANDIA TELA LA TREKTA LIKIWA
KWENYE MWENDO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO
ASJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA
RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISYONJE
BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA.GARI NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ONESMO S/O ANYANDULILE,MIAKA
57,KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA ISYONJE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO
HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE,VINGINEVYO ASJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed
By,
[DIWANI
ATHUMANI – ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon