“PRESS
RELEASE” TAREHE 26. 07.2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI
KUMGONGA MPANDA BAISKELI/
KUPOTEZA MUELEKEO NA KUWAGONGA WATEMBEA
KWA MIGUU NA GARI ILIYOEGESHWA PEMBENI NA
KUSABABISHA KIFO.
KWA MIGUU NA GARI ILIYOEGESHWA PEMBENI NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 25/07/2013 MAJIRA
YA SAA 13:00HRS HUKO UYOLE BARABARA
YA MBEYA/IRINGA GARI NO T 719 AUJ SCANIA
LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YUSTIS S/O KIBIKI, MIAKA 35, MBENA, NA MKAZI WA
MAKAMBAKO, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI
AITWAYE SIJALI S/O MICHAEL, MIAKA 25, MSAFWA, MKAZI WA UYOLE NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE PAPO HAPO NA KUPOTEZA MUELEKEO NA KWENDA KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI {1}
ANTONY S/O MSONGOLE, MIAKA 44, MMALILA, NA MKAZI WA UYOLE NA {2} EMMANUEL S/.O
MWASHUYA, MIAKA 20, MNYIHA NA MKAZI WA UYOLE NA KUWASABABISHIA MAJERAHA, KISHA
KULIGONGA GARI LILILOKUWA LIMEEGESHWA PEMBEZONI MWA BARABARA NA DEREVA AITWAYE
KAIMU S/O MUSA, MIAKA 35, MCHAGA, MKAZI WA UYOLE NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA
MALI. MAJERUHI WAMELAZWA KATIKA HOSPIATALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAANDALIWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO KUWA NA TAHADHARI
WANAPOENDESHA VYOMBO HIVYO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABANI ILI
KUEPUSHA AJLI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon