Miezi kadhaa baada ya kumbwaga Rihanna, mwimbaji Chris Brown aamua kumbwaga girlfriend wake mpya, Karrueche Tran.
Mwimbaji huyo amedai sababu ya kuachana
na girlfriend wake huyo mpya ni kwamba kwa sasa anahitaji kuwa single
ili kuweka mawazo yake yote kwenye kazi yake ya muziki.
Alipohojiwa na Hollywood Life, Chris Brown alisema;
“Mashabiki zangu wamekuwa wakiniona
kwenye mahusiano ya kimapenzi na wasichana tofauti tofauti, mnawajua ni
akina nani, lakini kwa sasa mimi kama mwanaume mwenye miaka 24, nimeamua
kuwa single.”
“Bado nina urafiki nao mzuri. Kwa
sasa nimeamua kuweka umakini wote kwenye muziki wangu kwani niko kwenye
kiwango changu cha juu kwa sasa.”
EmoticonEmoticon