TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

“PRESS RELEASE” TAREHE 02. 07. 2013.

 

WILAYA YA MBEYA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.

 MNAMO TAREHE 01.07.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA ILOMBA BARABARA YA MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI LENYE NO T.580 AZJ AINA YA STARLET LIKIENDESHWA NA DEREVA JAMES S/O ANGETILE, MIAKA 36, KYUSA, MKAZI WA UYOLE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ALEX S/O SANKE, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NJIA PANDA YA ILOMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO NI MWENDO KASI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI DEREVA HUYO ZINAFANYWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

 WILAYA YA MBARALI – AJALI YA POWERTILLER KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI

MNAMO TAREHE 01.07.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITAGE BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. POWERTILLER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA BARAKA S/O NIKOLAUS, MIAKA 19,MBENA MKAZI WA MBUYUNI LILIGONGA  PIKIPIKI T.441 BBW AINA YA SANLG ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MICHAEL S/O KIHOMWE,MIAKA 35,MHEHE,MKAZI WA MABADAGA NA KUSABABISHA KIFO CHA MWENDESHA PIKIPIKI HUYO PAMOJA NA ABIRIA WAKE  CHRISTINA D/O MANYALA,MIAKA 58,MSANGU,MKULIMA MKAZI WA MABADAGA PIA MAJERUHI KWA MWENDESHA POWERTILLER BARAKA S/O NIKOLAUS AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA  . MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. CHANZO NI DEREVA WA POWERTILLER KUSHINDWA KULIMUDU NA KUHAMIA UPANDE MWINGINE WA BARABARA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA RUNGWE – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

MNAMO TAREHE 01.07.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISYONJE WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.GEOFREY S/O MWAMBOJA, MIAKA 29, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA DSM NA 2. JACOB S/O GODSON, MIAKA 28, MMASAI, MKULIMA MKAZI WA ZANZIBAR WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] YENYE UJAZO WA LITA 02. WATUHUMIWA NI WANYWAJI WA POMBE HIYO TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA SAMBAMBA NA KUWA HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Signed By,

[BARAKAEL MASAKI - ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

 

Previous
Next Post »