Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu kwa ziara  ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani  Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.
Obama  ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji wake  rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu ya rais. NA MPEKUZI
Rais  Obama na mwenyeji wake wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja na  kisha Obama atafanya mazungumzo na waandishi wa habari kabla ya  kushiriki dhifa ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali hapo  baadaye Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha  hapo kesho Obama atatembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya  kuahidi kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme  Barani Afrika.
Mpango  huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi wake  wanakumbwa na matatizo ya upatikanaji wa umeme.
Karibu Barack Obama kanga pamoja na vitenge waliova wananchi wa waTanzania 
Katika  ziara yake Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika kusini na  hatimaye nchini Tanzania Obama amekuwa akisisitiza suala la demokrasia  ambapo ameeleza kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa kuwa na  viongozi wanaopambana kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha bora.
Katika  ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada za  kiongozi wa zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye ameeleza  kuwa jitihada zake za ukombozi kwa raia wa taifa hilo zilimsukuma  kuingia katika siasa na hatimaye kuwa rais wa kwanza mweusi nchini  Marekani

EmoticonEmoticon