Kim Kardashian ashawishiwa na mama yake kuuza picha ya mtoto wake kwa dola milioni 4!

The-Fashion-Tips-A-Pregnant-Kim-Kardashian-Will-Learn-From-Kourtney_s-Maternity-Style_0

LOS ANGELES

Mama wa staa Kim Kardashian, Kris Jenner,amemshawishi mwanaye kuuza picha ya kitoto chake kichanga kwenye chombo cha habari kwa dola milioni 4, Hollywood Life limeripoti.

Vyanzo vya karibu na staa huyo vimesema Kim amekuwa wazi kuuza picha ya kwanza kabisa ya binti yake (North West), lakini Kanye West amekuwa akipinga kuhusu suala hilo na kutaka utambulisho wa mwanaye kuwa siri.

Chanzo karibu na familia hiyo kinadai kwamba Kim anapingana na wazo la Kanye West huku akilinganisha hali yao na waliyokuwa nayo wakina Angelina Jolie na Brad Pitt, ambao waliuza picha za kwanza za wanao mapacha kwa dola milioni 15.

Previous
Next Post »