Mchungaji Vatikani asimamishwa kazi baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na rushwa.

20130628082635

 

Mchungaji mmoja amekamatwa kwa tuhuma za vitendo vya rushwa kuhusiana na uchunguzi mkubwa wa kashfa ilioikumba benki ya Vatikani.

Taarifa zinasema Mchungaji huyo Nunzio Scarano (pichani) kutoka Salerno amekamatwa baada ya uchunguzi wa Taasisi ya Kazi za Kidini ambavyo ndivyo benki hiyo inavyojulikana, kubaini tuhuma za kuwepo kwa mipango ya hujuma.

Mshauri Mwandamizi wa masuala ya vyombo vya habari wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatikani Greg Buke, amesema ripoti za awali zilizosema kwamba Scarano alikuwa ni askofu hazikuwa sahihi.

Msemaji wa Vatikan Federico Lombardi amesema mchungaji huyo amesimamishwa kazi kama mjumbe wa kamati ya usimamizi ambayo inashughulikia mali za Vatikani kama mwezi mmoja uliopita baada ya wakuu wake kugunduwa juu ya uchunguzi wa harakati zake.

Mchungaji Scarano alikamatwa pamoja na kachero wa zamani wa Italia na Mhasibu mmoja kwa madai ya kula njama za kuhamisha kiyume na sheria Euro milioni 20 kutoka Switzerland na kuzipeleka Italia.

Previous
Next Post »