Mbunge Mtwara Mjini Atiwa Mbaroni kwa Uchochezi

Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji Akamatwa na Jeshi la Polisi kwa Uchochezi

 



















 
 
 
 
 
 
 
Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein  Murji ametiwa mbaroni na Jeshi La Polisi kwa tuhuma za uchochezi na  kuhusika katika vurugu zilizotokea hivi karibuni katika viunga vya mji wa Mtwara.

Habari zilizoifikia habarimasai.com hivi punde zimeeleza kwamba mbunge huyo amekamatwa saa 2:30 jioni  hii na anashikiliwa katika kituo Kikuu cha Polisi Mjini Mtwara.

Katibu wa Mbunge huyo Meckland Millanzi amethibitisha kukamatwa kwa Murji na kwamba anahusishwa na mvurugu hizo.


Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso  amesema kwamba Murji amekamaywa hivi punde nyumbani kwake katika eneo la Shangani.

Taarifa zimebainisha kwamba Murji amekamatwa na kwamba hati ya kumkamata imeeleza anatuhumiwa kuchochea vurugu za kupinga gesi ya Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam.

Siku chache zilizopota zilizuka vurugu kubwa katika mji wa Mtwara na viunga vyake baada ya wananchi wa mji huo kuandamana baada ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa na Waziri wa wizara hiyo kueleza msimamo wa serikali kwamba mpango wa kusafirisha gesi jijini Dar es Salaam uko pale pale.


Awali kabla ya vurugu hizo kutokea shughuli mbalimbali za kijamii zilisimama huku watu wasiofahamika kusambaza vipeperushi kuhamasisha kusimama kwa shughuli hizo.

Kutokana na vurugu hizo baadhi ya watu walipoteza maisha, nyumba kuchomwa moto na madaraja kuharibiwa vibaya.

Mpaka sasa watu zaidi ya 80 wamekamatwa na jeshi la polisi na kushtakiwa mahakamani
Previous
Next Post »