Kampuni ya Tigo yashirikiana na The Guardian Limited kuzindua huduma ya Habari kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi.

 

IMG_1411

Mtaalamu wa Viwango wa kampuni ya Tigo Pamela Shelukindo (kushoto) akizungumzia kuzinduliwa kwa huduma ya ‘News SMS Service’ ambayo inalenga kuwapa habari wateja wa Mtandao wa Tigo popote pale walipo. Amesema huduma hiyo itakayokuwa ikipatikana kwa kutuma neon ‘GUARDIAN SMS na NIPASHE SMS itakuwa ikisimamiwa kiufundi na kampuni ya Premier Mobile Solutions (PMS). Katikati ni Meneja Mipango Msaidizi wa kampuni ya Premier Mobile Solutions Bi. Lulu Ramole na kulia ni Meneja Masoko Msaidizi Emmanuel Matondo.

IMG_1445

Meneja Mipango Msaidizi wa kampuni ya Premier Mobile Solutions Bi. Lulu Ramole (kulia) akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema huduma hiyo ya ujumbe wa habari kwa maandishi imetengenezwa kuwawezesha wateja kupata habari mara moja ambapo watumiaji wa mtandao wa Tigo watachajiwa mara moja kwa siku na kuweza kupata vichwa vya habari mara nne (4).

IMG_1437

Meneja Masoko wa Guardian Simon Marwa akifafanua kuwa ubunifu wa huduma ya habari kwa njia ya ujumbe wa maandishi katika simu ya mkononi bila shaka utawawezesha wasomaji wa magazeti ya ‘The Guardian’ na ‘Nipashe’ ambao pia ni watumiaji wa mtandao wa Tigo kupata habari mpya za uhakika kupitia simu zao za mkononi.

Previous
Next Post »