JENIFER KYAKA(ODAMA) AENDA NJE YA NCHI KUNUNUA VIFAA VYA KUTENGENEZEA FILAMU





                                    
 
 
 
 
Producer and actress Jenifer Kyaka(Odama) ameamua kwenda nje ya nchi kununua vifaa vya kisasa zaidi vya kutengenezea filamu na pia kupata elimu kuhusu utengenezaji wa filamu za kisasa kwa mujibu wa actress huyo mwenyewe. Odama ameamua ku-share picha akiwa Julius Nyerere international aiport tayari kwa safari hiyo akiwa na ndugu zake waliomsindikiza na kusema kuwa safari hiyo ina lengo la kuleta mapinduzi kwenye industry kwa kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE kuleta ushindani wa kuandaa filamu bora. "wadau wa filamu safari hii ni ya harakati za kuboresha kazi za kampuni kwa vifaa zaidi na elimu ya utengenezaji filamu za kisasa, kaeni mkao wa kipekee kabisa katika filamu za kampuni yetu zijazo, hakika tunakuja na ulimwengu mpya wa filamu" alisema actress huyo.

 Hii si mara ya kwanza kwenda nje ya nchi kununua vifaa kwani siku za nyuma pia aliwahi kufanya hivyo. Tunampongeza sana Odama kwa kuwa mpiganaji katika tasnia ambayo bado imetawaliwa na wanaume hasa katika uzalishaji na uongozaji wa filamu lakini tayari kampuni yake inafanya vizuri. Angalia picha akiwa uwanja wa ndege tayari kuanza safari yake katika nchi ambayo hakuitaja.
Previous
Next Post »