Vurumai zilizuka kati ya wabunge wa Venezuela siku ya Jumanne usiku ambapo zilisababisha kiasi mbunge mmoja wa upinzani kuumizwa vibaya na kutokwa na damu.
Wabunge wa serikali walianza kuvurumisha ngumi baada ya wabunge wa muungano wa upinzani kufungua bango bungeni wakipinga marufuku iliyowekwa baada ya uchaguzi , ambayo imesababisha kuvuliwa kwa uwezo wa ubunge kwa wengi wa wabunge wa upinzani.
Upande wa upinzani umesema kuwa kiasi ya wabunge 17 ambao ni washirika wao na wabunge watano wanaounga mkono serikali wamejeruhiwa. Wabunge wanaounga mkono serikali walijitokeza katika televisheni wakiwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuwashambulia.
EmoticonEmoticon