Mume, mkewe kortini wakidaiwa kuwatesa watoto

Dar es Salaam. Mfanyabiashara na mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam, Omary Maneno (36) na mkewe Judith Lucas ama Lea (28) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuwapiga watoto wao kwa kutumia fimbo na mabomba.
Akisoma hati ya mashtaka jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka alidai kuwa Februari 2013, Maneno na mkewe Judith, ambaye ni mama wa kambo wa watoto wa kike wenye umri wa miaka 7 na 5 waliwapiga kwa kutumia fimbo na mabomba na kuwasababisha maumivu makali mwilini.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 169 (1) na (2) cha sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Iliendelea kudai kuwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Bunge, Wilaya ya Ilala wakati mdogo wake mwenye umri wa miaka mitano ni mwanafunzi wa chekechea shuleni hapo.


Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika
Previous
Next Post »