Alhaj Mwinyi ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na asasi ya Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) kwa ajili ya kuchangisha fedha za ujenzi wa makazi ya wazee jijini Dar es Salaam yatakayogharimu shilingi milioni 300.
Amesema kukithiri kwa ubinafsi miongoni mwa wananchi kumesababisha wazee kukosa huduma muhimu ikiwemo malazi, mavazi, huduma za afya pamoja na chakula cha uhakika na hivyo wengi wao kuamua kukimbilia mitaani na kugeuka kuwa ombaomba.
|
ALHAJI ALI HASSAN MWINYI- Rais Mstaafu Tanzania |
Ameyaomba mashirika na watu binafsi kuunganisha nguvu zao na kujitoa kwa hali na mali katika kuchangia maendeleo ya wazee kwani wazee ni rasimali, kielelezo cha hekima bora na ngao kwa taifa na kwamba taifa lisilothamini wazee ni sawa na kupoteza historia, mila na utamaduni wake.
|
BALOZI JUMA MWAPACHU - AKISIKILIZA KINACHOENDELEA KWENYE MKUTANO HUO.
|
Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Tushikamane Bi Rose Mwapachu na mlezi wa asasi hiyo Bi Aisha Bilal walisema kwamba asasi hiyo imekwishawafikia wazee 36 jijini Dar es Salaam tangu kuanzishwa kwake ambapo wamekuwa wakitoa misaada ya kibinadamu ikiwemo lishe, mavazi na huduma za afya kila mwezi.
|
ROSE MWAPACHU - Mkiti TPF |
|
AISHA BILAL - Mlezi TPF |
|
WADAU MBALI MBALI WAKITETA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO |
EmoticonEmoticon