SAKATA LA VURUGU ZA MACHINGA NA POLISI IRINGA ,MTANGAZAJI WA NURU FM AKAMATWA

 





Wafanyakazi  wa  radio  Nuru  FM  wakiwa katika  kikao 
SAKATA  vurugu  za  machinga na polisi mjini Iringa limechukua  sura  mpya  baada ya  jeshi la  polisi kumkamata  mtangazaji  wa kituo cha Radio Nuru FM Husein Farahan wakati akiwa njiani kuelekea  kazini.

Mtangazaji  huyo amekamatwa asubuhi  ya  leo  wakati akielekea kazini hata  hivyo  mtangazaji  huyo anadaiwa  kupigwa  virungu na jeshi la polisi  wakati akikamatwa  pamoja na watu wengine 60 akiwemo  mbunge wa  jimbo  hilo mchungaji Peter Msigwa.
Previous
Next Post »