Rupia Banda azuiwa uwanja wa ndege

Zambia. Aliyekuwa Rais wa Zambia, Rupia Banda amezuiwa kwenda kushuhudia sherehe za kumwapisha   Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta jana.
Rais huyo wa zamani Rupia Banda anakabiliwa na mashtaka  ya matumizi mabaya ya madaraka nchini Zambia.
Kwa mujibu wa  mwanasheria wake Rupia Banda alizuiwa kutoka nchini humo kutokana na kukabiliwa na kesi hiyo ambapo hatakiwi kutoka nje ya nchi yake.
Banda anayekabiliwa na kesi hiyo alirudishwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege uliopo mjini Lusaka akijiandaa na safari kuelekea Kenya.
Alizuiliwa na ofisa wa uhamiaji wa uwanja wa ndege kwa sababu haruhusiwi kutoka nje ya nchi hiyo kutokana na kesi yake inayomkabili.
Mwanasheria  Robert Amsterdam alisema kwamba hati ya kusafiria ya Banda ilikuwa chini ya ulinzi wa mahakama kama sehemu ya dhamana yake.
Alisema kwamba Rais huyo alikuwa anataka kwenda kushuhudi kuapishwa kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliyeapishwa jana.

Kutokana na kesi hiyo inayomkabili Rais wa zamani, Rupiah Banda alisema hana hatia katika kesi hiyo.
Mashtaka anayokabiliwa nayo Banda yamehusishwa na mkataba alioidhinisha kati ya nchi hiyo na Nigeria kuhusu uuzaji wa mafuta ambapo waendesha mashtaka walisema ulinuia kumfaidisha  Banda na familia yake.
Rais huyo wa zamani alisema kuwa mashtaka hayo ni sehemu ya njama za kisiasa dhidi yake na washirika wake.
Baada alishindwa na mpinzani wake Michael Sata katika uchaguzi mwaka 2011.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa Banda na mwanaye Henry Banda waliweka pesa katika akaunti za kigeni, pesa zilizotokana na mkataba wa mafuta kati ya Zambia na Nigeria. Pesa hizo inadaiwa zilitumika kufaidisha familia ya Banda
Previous
Next Post »