NI KWELI WIZI SI KITU KIZURI TUACHE KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUIBA.



Kijana Aliyepata kipigo kutoka kwa wananchi akionekana akilia
Kijana anayedaiwa kuiba akiwa chini akiugulia maumivu baada ya kupata kichapo.

Kijana mwenye hasira akiwa amemshika kijana anayedaiwa kuwaibia.


Kijana ambaye jinalake halikufahamika mara moja amenusurika kufa baada ya kupata kipigo kwa wasamaria wema kwakile walichodai kuwaibia kijana huyo kuwaibia Power window za magari huko migombani Street katika eneo la mikocheni jijini Dar es Salaam.

Katika sakata hilo la wizi uliokuwa ukimkabili kijana huyo vijana wa 4C NINJAS ambao wao ndio walikuwa walinzi wa eneo hilo walisema walipo mkamata kijana huyo kwa wizi wananchi wenye hasira walionekana kujawa na jazba ndipo wakatoa kipigo kwa kijana huyo kama onyo kwa wengine.

Hata hivyo kijana huyo awali ambaye inaelezwa alikuwa akiranda randa katika eneo hilo ambapo watu walimstukia kama mwizi baada ya kumkamata na kumpa kipigo alidai ametoka kazini jambo ambalo liliwakera hadi wamiliki wa magari hayo kwani eneo hilo walishawahi kuibiwa tena jambo ambalo liliwatia hofu.

Aidha hadi naondoka eneo hilo mtuhumiwa huyo alikuwa kawekwa chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wakilinda mabac ya summry.

Previous
Next Post »