Mrembo huyu aliyejitambulisha kwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimojawapo mjini Iringa akilia baada ya kupokea kichapo kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara eneo la Miyomboni mjini Iringa baada ya kuiba viatu vya mtumba na kuficha kwapani
Hapa akimpigia simu mpenzi wake ili aweze kumkomboa baada ya kutakiwa kulipa Tsh 50,000 kwa viatu pea mbili alizoiba .
Tukio la mrembo huyo kupokea kichapo na kuvuliwa nguo na kupokonywa simu yake na mikoba zaidi ya mitano pamoja na kiasi cha TSh 15,000 ambazo alikuwa amezihifadhi limetokea jumapili wiki hii katika eneo la Miyomboni mjini Iringa.
Akielezea juu ya mkasa huo wa aina yake leo mfanyabiashara huyo mama Masawe alisema kuwa eneo hilo amekuwa na kawaida ya kuibiwa viatu katika duka lake la viatu vya mtumba .....
Mama huyu anadai kuwa mbali ya kukamatwa kwa mrembo huyo bado amepata kukamata vijana zaidi ya wawili watanashati ambao wamekuwa wakifika na kujifanya wakichagua viatu na kuishia kuiba na kutoweka .
Binti huyo ambaye ni mwanachuo alifika dukani hapo na kuanza kuchagua viatu akijifanya ni mteja .....
Baada ya kuona muuza duka ameangalia pembeni, binti huyo alichukua pea moja ya viatu na kuificha kwapani asijue kwamba pembeni kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akimwangalia....
Alipoaga na kutaka kuondoka ndipo timbwili la kichapo lilipoanza kwa mrembo huyo ambae aliomba asipelekwe polisi na asipewe adhabu kubwa kwa kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu tumboni.
Alisema kuwa kutokana na maombi ya mrembo huyo kupunguziwa adhabu hakuweza kumfikisha polisi zaidi ya kumpa kichapo cha kufa mtu na kumpokonya mali zote alizokuwa ametoka kuiba katika maduka ya Miyomboni mjini hapa pamoja na simu yake ya kiganjani .
EmoticonEmoticon