CAPTURADO APIGWA NA WAISLAM WENYE SIASA KALI

CAPTURADO APIGWA NA WAISLAM WENYE SIASA KALI

MCHEZA filamu nyota hapa nchini, Simon Mwakipagata “Capturado” juzi usiku alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya na waislam wenye siasa kali.
Rado aliiambia Saluti5 kuwa wakati akiendesha gari lake maeneo ya Mwananyamala jirani na mskiti wa Taqwa ndipo masahibu hayo yalipomfika.
“Nikutana na kundi kubwa likiwa linampiga kibaka, kundi hili lilikuwa limeziba njia, nikaamua kuwapigia honi mara kadhaa ili wanipishe.
“Badala ya kunipisha walianifuata na kuanza kunishambulia na hatimaye kunitoa kwenye gari, walinipiga sana na baadae sikuelewa kilichoendelea hadi nilipojikuta nipo hospitalini.”
Rado anasema baadae aliambiwa kuwa watu wale walikuwa ni waumini wa msikiti wa Taqwa ambao walikuwa kwenye operesheni ya kuwasaka wezi wa simu ya mmoja wa viongozi wa msikiti huo.
Aidha Rado ambaye ameruhisiwa na kurejea nyumbani, alisema gari lake lipo salama.
Previous
Next Post »