Maelfu ya waumini watafurika katika uwanja wa mtakatifu Petro leo kumuaga kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Benedikti wa 16, wakati atakapoongoza misa yake ya kwanza tangu alipotangaza Jumatatu iliopita kuwa anajiuzulu.
Papa, mwenye umri wa miaka 85, alisema ataacha wadhifa huo tarehe 28 mwezi huu kwa sababu ya umri. Baada ya misa hiyo leo mchana atakuwa na misa nyengine kwenye Kanisa kuu la mtakatifu Petro alasiri, moja wapo ya shughuli zake za mwisho akiwa kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki.
Uongozi wake wa miaka minane ni moja kati ya vipindi vifupi katika Kanisa hilo. Wakati huo huo, makadinali wa ngazi ya juu wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya leo wakati wakikusanyika mjini Roma kumchagua papa mpya kuwaongoza waumini bilioni 1.2 wa Kikatoliki duniani.
Bado hakuna tarehe iliyopangwa kwa mkusanyiko huo ambao ni wa faragha

EmoticonEmoticon