Rais wa Marekani Barack Obama, emeelezea nia yake ya kuufufua
uchumi wa Marekani, na kuufanya thabiti katika hotuba yake ya kwanza tangu
kushinda muhula wa pili wa urais.
Obama alisema kuwa alitaka kuinua maisha ya wamarekani maskini , kufanya mageuzi katika idara ya uhamiaji, kusawazisha mishahara kwa wanawake na wanaume na kupandisha mapato kwa wamarekani wa kipato cha kadri.
Aliahidi kuwasha upya kile alichokiita Injini ya kukuza uchumi wa nchi ambao ni wananchi wa kipato cha kadri.
Alilitaka bunge la Congress,kushirikiana naye kuweza kupunguza madeni ya nchi hiyo,kudurusu sheria za utoaji wa kodi kwa matajiri na kubuni nafasi za kazi.
Pia alishinikiza bunge la Congress kuhusu kura ya kudhibiti sheria za umiliki wa bunduki jambo ambalo wengi walilishangilia sana.
Alikuwa anagusia kisa cha msichana mmoja aliyeuawa baada tu ya sherehe za kuchaguliwa kwake kwa muhula wa pili mwezi Januari.
Obama pia ametangaza kuwa wanajeshi elfu thelathini na nne wa Marekani wanaohudumu Afghanistan watarejeshwa nyumbani mwaka ujao.
Aliongeza kuwa vita vya Afghanistan vitaisha kufikia mwisho wa mwaka ujao.
Wakati huo huo tangazo la Obama kuwa atawapunguza wanajeshi wake kwa unusu nchini Afghanistan zimepokelewa vyema na serikali ya Afghanistan.
Hata hivyo kundi la Taliban limeonya kuwa hata kukiwa na mwanajeshi yeyote wa kigeni Afghanistan itamaanisha kuwa mapigano yataendelea.
Katika mawasiliano ya simu na Rais Obama kabla ya hotuba hiyo, Rais wa Afghanstan Hamid Karzai alieleza umuhimu wa kusawazisha usalama na uhuru wa Afghanistan.
Mwandishi wa BBC huko Kabul anasema kuwa bado kuna hofu kuhusu ikiwa wanajeshi wa Afghnistan wako katika nafasi bora ya kuzuia mashambulizi kutoka kwa wapiganaji ikiwa wanajeshi wa Marekani wataondoka.
EmoticonEmoticon