Mabango ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2008
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe amejiuzulu kwa sababu
za kiafya
Hatua ya Bwana Simpson Mutambanengwe, inakuja huku Zimbabwe ikijiandaa kwa
kura ya maoni kuhusu katiba mpya pamoja na uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka
huu.
Waziri mkuu Morgan Tsvangirai, amekuwa akishinikiza kufanyika mageuzi katika
tume ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwepo uchaguzi huru na wa haki.
Uchaguzi huo utakuwa ishara ya kumalizika kwa utawala wa serikali ya Muungano
iliyoundwa baada ya ushindi wa Rais Robert Mugabe katika uchaguzi uliofanyika
2008 na uliokumbwa na ghasia na vurugu.
Bwana Tsvangirai, kiongozi wa chama cha MDC alisusia duru ya pili ya uchaguzi
mwaka huo baada ya kudai kuwa alipokonywa ushindi wake katika duru ya
kwanza.
Tsvangirai pamoja na Mugabe wanatarajiwa kugombea urais katika uchaguzi
huo.
Chama cha Rais, Mugabe, Zanu-PF, pia kilidaawa kufanya ghasia dhidi ya
wafuasi wa upinzani, madai aliyoyakanusha.
Waziri wa sheria, Chinamasa, alisema kuwa Mugabe alikubali kujiuzulu kwa
Bwana Mutambanengwe, ambaye ni jaji mstaafu, aliyechukua wadhifa huo baada ya
uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2008.
"sababu za kiafya ndizo zimempelekea kujiuzulu,'' alisema Chinamasa
Mrithi wa Mutambanengwe, atateuliwa baada ya majadiliano kati ya viongozi wa
serikali ya Muungano.
Mwezi jana shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch,
liliitisha mageuzi katika tume ya uchaguzi , idara ya mahakama na vyombo vya
habari likidai kuwa zinaunga mkono chama cha Zanu PF
EmoticonEmoticon