Binti augua Ugonjwa wa ajabu



FLORIDA, Marekani
HAKIKA hujafa haujaumbika, msemo huu unaweza kuufananisha na tukio lililomsibu mwadada Amanda Gryce kutoka kule nchini Marekani baada ya kukumbwa na ugonjwa ajabu.
Wengi wanaweza wakasema kwamba anapata raha, lakini sio kweli kwani ugonjwa huu unamtokea sehemu yoyote ambapo haustahili kumtokea mtu wa kawaida hali ambayo kwa mujibu wake inamsababishia karaha.
Inafahamika kwamba kuishi maisha ya kupenda ngono kupita kiasi kwa wengi wetu ni maisha mabaya na yasiyofaa, lakini kwa Amanda Gryce si jambo la ajabu.
Binti huyu mwenye umri wa miaka 22 anasema, maisha yake yameharibiwa na mfumo wa homoni zake za mwili ambapo anaweza kufikia mshindo mara kwa mara anaposikia sauti za aina fulani.
Anasema sauti ya muziki, magari yanapotembea, treni na hata milio ya simu ni kati ya vitu vinavyomfanya kufikia hali hiyo mara kwa mara na kusababisha ashindwe kuwa huru katika maisha yake.
Hiyo inamtokea mara kwa mara iwapo anakuwa na marafiki zake na hata anapokuwa kazini kwake kama mkusanyaji wa mauzo kwenye duka la bidhaa za watoto huko Florida nchini Marekani.
Tatizo hilo linalomkumba Amanda ni nadra sana kutokea katika mwili wa binadamu hasa wanawake. Tatizo hilo liitwalo Persistent Sexual Arousal Syndrome (mwili kuendeleza masuala ya usisimuaji) au PSAS limesababisha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Kwa mujibu wa Amanda anasema tatizo hili alianza kukumbana nalo alipokuwa na umri wa miaka minane tu, na sasa limekuwa tatizo sugu kwake.
Ingawa tatizo hili la PSAS ni nadra kutokea, inaweza kuwa na madhara makubwa kwa watu wachache ambao wanakabiliwa na hali hii.
Mwaka 2012, Gretchen Molannen 39, aliyekuwa akiishi Florida nchini Marekani, aliamua kujiua baada ya kuishi na tatizo hilo kwa miaka 16.
Tatizo hili limekuwa gumu pia kwa Amanda ambaye naye anaishi katika mji huohuo wa Florida, lakini binti huyu yeye anasema mara nyingine amekuwa akiamua kujichua hata mara 15 kwa siku moja ili kuweza kupata unafuu.
Anasema, “Sipati raha yoyote unaweza kusema kuwa yamekuwa ni mateso. Hali hii inakuwa inaongoza maisha yako ya kila siku na ni kama kuishi katika ndoto.

Previous
Next Post »