Watu watatu wameuawa na mtu aliyekuwa na bunduki katika kijiji cha Kusini mwa Uswisi, Daillon. Polisi wamesema watu wengine wawili wamejeruhiwa katika tukio hilo. Mtu huyo aliyekuwa na silaha amelazwa hospitalini kufuatia makabiliano ya risasi na polisi katika eneo la tukio.
Mwanamume huyo inadaiwa alikuwa mlevi kupindukia kabla ya kuanza kufyatua risasi. Taarifa ya polisi iliyotolewa mapema leo haijatoa maelezo zaidi kuhusu kiwango cha mejeruhi, na hakuna habari yoyote kuhusu sababu ya ufyatuwaji huo wa risasi.

EmoticonEmoticon