Rais Obama aidhinisha mswada wa kifedha

 
Rais wa Marekani, Barack Obama, ameutia saini na kuwa sheria mswada uliopitishwa na bunge juu ya kuiepusha nchi hiyo kutokana na mchanganyiko wa hatua zilizotishia kuiingiza katika mdororo wa uchumi. Hatua hizo zilikuwa zianze kutekelezwa Januari mosi.

 Sheria iliyotiwa saini na Obama inaruhusu kupandisha kodi kwa Wamarekani tajiri, na pia itawezesha kuahirisha hatua ya kukata matumizi ya serikali kwa muda wa miezi miwili.

Wataalamu walihofia kwamba kumalizika kwa muda wa kukata kodi kwa walipa kodi wote, sambamba na kukata matumizi ya serikali kungelikuwa pigo kwa uchumi wa Marekani kutokana na kusababisha pengo la dola billioni 600 bila ya kupandisha kodi.
Mazungumzo ya dakika za mwisho mwisho katika Baraza la Seneti na Baraza la wawakilishi Jumanne iliyopita yalifikia makubaliano.
Previous
Next Post »