Mwaka umeanza poa sana na wasanii wengi walifunga mwaka na ngoma kali na wengine kufungua mwaka na ngoma kali vilevile, lakini January 11 inaweza kuwa siku ambayo fans wa bongo fleva wataifaidi ladha mpya kabisa ya muziki toka kwa wasanii wawili, stamina na Vanessa Mdee.
Vanessa Mdee Yule aliyeung’arisha wimbo wa Ommy Dimpoz “Me and You” pamoja na “Money” ya AY, mtangazaji wa MTV Base na Choice FM ya Tanzania anatarajia kuachia wimbo wake wa kwanza kabisa unaoitwa ‘CLOSER’,ukiwa umepikwa katika studio za B’Hits chini ya Pacho Latino na Hermy B. Na kwa mujibu wa watu waliopata nafasi ya kuusikiliza wanasema ni bonge la ngoma.
Stamina |
Kwa upande mwingine chanzo chetu cha kuaminika kilipiga story na STAMINA ambae ni msanii aliyefanya vizuri sana mwaka 2012, na kwamba yeye anatarajia kuileta ladha mpya kabisa kwa fans wake kwa kuachia ngoma aliyofanya na msanii ambae yeye mwenyewe anamkubali hadi kuurudia wimbo wake wa Mwanza Mwanza na anasema ndiye role model wake, yaani Fid Q. Wimbo unaitwa“Toleo Jipya” umepikwa katika studio za bongo records chini ya producer of his dream P. Funky Majani.
Katika interview aliyofanya na Lucas Maziku wa radio SAUT hivi karibuni Stamina alisema ilikuwa auachie wimbo huo mapema sana mwezi huu , na kuongeza kuwa mwisho wa mwezi huu anaachia album yake ya kwanza inayoitwa“ALISEMA”. Lakini amesogeza mbele kidogo tarehe za kuachia wimbo huo na sasa ni January 11.
EmoticonEmoticon