Uwindaji umepigwa marufuku Zambia


simba

Serikali ya Zambia imepiga marufuku uwindaji wa Simba na Chui kufuatia kupungua kwa idadi ya wanyama hao nchini humo.

Waziri wa utalii wa Zambia, Sylvia Masebo, amesma serikali ya nchi hiyo inapata dhamana kubwa kutokana na ziara za watalii katika mbuga za wanyama kuliko shughuli za uwindanji ambayo iliipa serikali dola milioni tatu pekee mwaka uliopita.

Masebo amesema kwa sasa taifa hilo halina idadi ya wanyama hao ili kuruhusu uwindaji zaidi.

Chui

''Watalii huja Zambia, kutizama Simba na ikiwa tutawapoteza wanyama hao kwa kuwauawa basi tutakuwa tumekandamiza secta ya utalii'' alisema waziri huyo.

Idadi ya Simba katika mbuga za wanyama nchini humo imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwandaji.

Inakadiriwa kuwa kuna takriban Simba 4,500 nchini Zambia huku idadi ya Chui ikiwa haijulikani.

Nchi jirani ya Botwana imetangaza kuwa mchezo wa uwindaji utapigwa marufuku kuanzia mwaka wa 2014 nayo Kenya ambayo imenufaika pakubwa na shughuli za kitalii ilipiga marufu uwindaji miongo kadhaa iliyopita.
Previous
Next Post »