Mshukiwa mmoja wa udakuzi wa komputa ambaye anasakwa na idara
ya ujasusi nchini Marekani, FBI, kuhusiana na madai ya kuiba mamilioni ya madola
kutoka benki za Marekani, ili kufadhili maisha ya anasa, amekamatwa mjini
Bangkok Thailand.
Shirika hilo la FBI, limekuwa likimsaka mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24, Hamza Bendelladj, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya komputa, kutoka Algreia kwa zaidi ya miaka mitatu.
Polisi nchini Thailand wanasema mshukiwa huyo, Bendelladj amekiri alitumia fedha hizo kuisha maisha ya starehe na anasa.
Bendelladj, anazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi katika uwanja wa ndege mjini Bangkok baada ya kuwasilia kutoka Malaysia akiwa safirini kuelekea Misri.
Utawala wa Marekani unamtuhumu kuhusika na wizi katika akaunti za watu binafsi katika zaidi ya mabenki 217 na taasisi wa kifedha kote duniani na kusababisha hasara ya mamilioni ya madola.
Mkuu wa polisi nchini Thailand amesema mshukiwa, alikamatwa katika uwanja mkuu wa ndege ambako alisema yeye pamoja na familia yake wamekuwa likizoni.
Polisi wanasema wamenasa komputa mbili, kifaa kimoja cha tarakilisha, simu ya sate lite na vifaa vingine vya komputa kutoka kwa mshukiwa huyo.
Ripoti zinasema Bendelladj anatarajiwa kusafirishwa hadi nchini Marekani, katika Jimbo la Georgia ambako mahakama moja ilitoa kibali cha kukamatwa kwake.
ndelladj anatarajiwa kusafirishwa hadi nchini Marekani, katika Jimbo la Georgia ambako mahakama moja ilitoa kibali cha kukamatwa kwake.
EmoticonEmoticon