Wabunge wa muungano mkuu wa wabunge wasioegemea upande wowote
katika serikali ya mseto nchini Libya, wamejiondoa na kutangaza kuwa
hawatahudhuria vikao vya bunge kulalamikia kucheleweshwa kwa shughuli ya
kuandika katiba mpya, ili kuongoza nchi hiyo, baada ya kuondolewa na kuuawa kwa
kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muamar Gadaffi.
Mbunge mmoja wa muungano wa Liberal National Forces Alliance (NFA) Souad Sultan, ameiambia BBC kuwa bunge hilo limeshindwa kuafikia matakwa na matarajio ya raia wa nchi hiyo.
Bunge hilo ambalo lilichaguliwa mwezi Julai mwaka uliopita, miezi Tisa tangu kuuawa kwa Kanali Muammar Gaddafi.
Sultan amesema kuwa wabunge wameshindwa kukubaliana kuhusu jinsi katiba hiyo mpya inapaswa kuandikwa.
Mwandishi wa BBC, katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, Rana Jawad, anasema kuwa muungano huo wa NFA utaka wapiga kura kuchagua kamati ya watu 60, ambao watahusika na shughuli ya kuandika katiba hiyo mpya.
Lakini, makundi mengine yanataka bunge hilo lenye wanachama mia mbili kuchagua kamati hiyo.
Muungano wa NFA, ambo ndio mkubwa zaidi katika bunge la nchi hiyo, pia umesema ukosefu wa usalama na jinsi bunge hilo linavyoendesha ndio sababu kuu ya wao kujiondoa.
Wabunge wa muungano huo wamedhulumiwa mara kadhaa katika meizi ya hivi karibuni, baada ya waandamanaji kuvamia bunge hilo, na kutatiza vikao vyake.
Lakini mbunge mmoja wa chama cha Minority Front Party, MFP, Mohamed Addarat, amesema kujiondoa kwa wabunge wa NFA hakutakua na athari yoyote, katika shughuli za bunge hilo.
Amesema bunge hilo litaendelea na vikao vyake bila tatizo lolote.
Ibrahim al-Gheriani, ambaye ni kiongozi wa muungano huo wa NFA, amesema wamegadhabishwa na utendaji kazi wa bunge hilo.
Lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari, wabunge wa muungano huo wanatarajiwa kurejea tena bungeni baadaye wiki hii.
Libya imekubwa na msukosuko wa kisiasa tangu kuondolewa madarakani na kuuawa kwa Kanali Muammar Gaddafi Oktoba mwaka wa 2011.
Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikijaribu kuwapokonya silaha makundi ya wapiganaji ambayo yamekuwa yakijaribu kupambana na wanajeshi wa serikali ya sasa.
EmoticonEmoticon