Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuwatumia
wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko ughaibuni
(Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye umuhimu kwa
Taifa.
Hapo awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine,
ambapo kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika pale
tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi hawajapatikana
kufanya kazi husika.
Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa
Kitanzania kwenye maeneo yafuatayo:-
1.Mfumo mzima wa utafutaji,
uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia na mafuta.
2.Kuimarisha matumizi
salama ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji
wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
3.Kuboresha utekelezaji wa
malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha
tunapata matokeo makubwa na ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati
katika maendeleo ya Taifa.
Wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini
katika maeneo haya, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza
kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha.
Mwito unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ughaibuni
au ndani ya nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s) pamoja na maelezo ya
kwa nini wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta. Tumia anuani
ifuatayo:-
Katibu Mkuu
EmoticonEmoticon