Kiongozi wa Google-atembelea Korea ya kaskazini


Mkuu wa kampuni katika mtandao wa Internet ya Google , Eric Schmidt , yuko ziarani nchini Korea ya kaskazini. Akiwa pamoja na gavana wa zamani wa jimbo la New Mexico nchini Marekani, Bill Richardson, anataka kufahamu juu ya masuala ya kiuchumi na vyombo vya habari katika nchi hiyo ya kikomunisti. Schmidt ni mwakilishi pekee hadi sasa wa masuala ya kiuchumi ambaye amewahi kuitembelea Korea ya kaskazini hadi sasa. Katika nchi hiyo yenye usiri mkubwa mtandao wa internet unadhibitiwa vikali. Wengi wa wananchi wa Korea ya kaskazini hawana uwezo wa kuingia katika mtandao wa internet. Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imekosoa ziara hiyo na kusema kuwa hana maana.
Previous
Next Post »