Jeshi la Misri lazuwia shambulio dhidi ya kanisa

 
Jeshi la Misri limezuwia mapema leo shambulio dhidi ya kanila la Wakristo wa madhehebu ya Koptic katika mji wa mpakani na eneo la Gaza wa Rafah, wakati waumini hao ambao ni wachache nchini humo wakianza sherehe za Krismas leo.

Shirika la habari nchini Misri limesema kuwa vikosi vya jeshi vimezuwia shambulio dhidi ya kanisa katika mji wa Rafah na kukamata gari iliyokuwa imewekwa miripuko na silaha karibu na kanisa hilo.

Gari nyingine iliyokuwa na watu waliojifunika nyuso zao ilikimbia wakati askari hao wa doria walipoikamata gari hiyo iliyojaa miripuko.
Wakristo wa madhehebu ya Koptic nchini Misri ambao ni wachache wanasherehekea sikukuu yao ya kwanza ya Krismasi chini ya utawala mpya wa vyama vinavyoongozwa na Waislamu huku kukiwa na hali ya hofu na hali isoyoeleweka ya baadaye nchini humo.

Mwezi Septemba , wakaazi na maafisa wameripoti kuwa familia kadha za waumini wa Kikoptic kutoka Rafah walikimbia kutoka katika mji huo ulioko katika rasi ya Sinai ambayo inapakana na ukanda wa Gaza baada ya kupata vitisho kutoka kwa makundi ya Kiislamu.
Previous
Next Post »